User:Josles
DR JOHN POMBE MAGUFULI, SHUJAA, MWANAMAPINDUZI NA NGUZO YA MABADILIKO YA KIUCHUMI, KIUTAMADUNI NA KIJAMII KATIKA KARNE YA 21.
Historia ya Bara la Afrika katika Karne ya 21 ina mambo mengi ya Kuandika kuhusu Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Historia ya Shujaa Huyu itaangazia namna alivyoweza Kujenga Mfumo Imara wa Kifikra kwa Viongozi na Wananchi wa Bara la Afrika wa Kuamini kuwa Bara la Afrika linaweza Kujenga Uchumi wake bila kutegemea misaada toka Nchi za Kibepari.
Kupitia Raslimali zilizopo Barani Africa, Dr John Pombe Magufuli amekuwa akiongoza kwa mifano kwa viongozi wa Bara la Afrika namna haswa wanavyopaswa kusimamia maslahi ya Wananchi wao na kuhakikisha wananufaika na Raslimali hizo. Wakati wa Sakata la Makinikia Nchi nyingi za Afrika zilikuwa zikitizama kwa uoga kuhusu maamuzi yale magumu ya Dr. John Pombe Magufuli. Baada ya Kufanikiwa kuingia makubaliano na Kampuni ya Barick yenye kulenga kuwanufaisha Wananchi wa Tanzania ndipo hapo Viongozi wa Nchi Mbalimbali za Afrika walipoona kuwa inawezekana kabisa Wananchi kunufaika na Raslimali zao kama madini, Mbuga za Wanyama, Ardhi, na vyanzo mbalimbali vya Maji.
Msimamo wa Dr John Pombe Magufuli kukataa kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kwa masharti ya Kinyonyaji ambayo yalitaka Wachina wawekeze kujanga Bandari hiyo kisha waimiliki kwa miaka 33 bila kulipa Kodi na bila kuwa na udhibiti wa Serikali ya Tanzania, Kisha Ardhi ya Bandari kuwa chini ya umiliki wa Wachina kwa miaka 99 na masharti mengine ya Kiuwendawazimu ndipo hapo Nchi nyingine za Bara la Afrika zilianza kutilia shaka mikataba inayotekelezwa na nchi za Kibepari. Ujasiri huu wa Dr. Magufuli ni uthibitisho wa kuwa alijitoa sadaka kuwapigania Mamilioni ya Watanzania wa Wa Afrika kwa Ujumla.
Dr. Magufuli aliamini katengeneza Mifumo itakayotengeneza Fursa za Kujitengenezea Kipato kwa watu wengi kuliko Kutengeneza kizazi kinachotegemea Ajira kwani alijua wazi kuwa hakuna Nchi inaweza kumaliza tatizo la Ajira. Katika Kufanya hivyo aliwekeza Nguvu kubwa katika Kujenga Miundombinu Bora ambayo kila mwenye akili timamu angeweza Kujitengenezea Kipato kupitia hiyo. Tafakari maisha yatakuwaje baada ya Kukamilika Miradi yote ya Kimkakati aliyoianzisha. Bara zima la Afrika liliona kuwa Dr Magufuli alichagua njia ya Kutengeneza Fursa za Kiuchumi kuliko Kutengeneza kizazi tegemezi cha kuwa vibarua kwenye Miradi ya Kinyonyaji inayotekelezwa na Mataifa ya Kigeni.
Dr. John Pombe Magufuli alipinga hadharani utumwa wa Kifikra uliowekwa na wazungu kwa miaka mingi wa Kuamini kuwa Lugha na hata tamaduni zao ni Bora katika Bara la Afrika. Mchango wa Dr. Magufuli katika ukuaji wa Lugha ya Kiswahili Duniani haupimiki na utadumu milele katika akili za Waafrika kote Duniani. Lakini pia msimamo wa Dr. Magufuli kuhusu Chanjo ilikuwa kielelezo tosha kuwa alitamani kuona siku Moja Bara la Afrika likiweza kuwa na Njia zake za kushughulikia masuala yake ya kiafya kupitia wataalamu wake na Teknolojia zilizotengenezwa Afrika.
Hakika tutakukumbuka Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Mwanaharakati wa Masuala ya Kiuchumi, Mwana mzalendo wa Bara la Afrika. Shujaa uliyeamua kusimamia maslahi ya Wananchi..... Mwanafalsafa ambaye mawazo yako yataishi Daima.
Pumzika kwa Amani Baba Magufuli.
Josias Charles